Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Uchafuzi wa Hewa

Maswali yoyote uliyowahi kuwa nayo kuhusu aina hii ya uchafuzi sugu yajibiwa kwa pamoja na wanasayansi.

 

  1. KWA NINI UCHAFUZI WA HEWA NI SUALA LINALOHITAJI KUPEWA KAPAUMBELE?

Uchafuzi wa hewa umetuzunguka. Watu wengi duniani wanaishi kwenye sehemu zenye kiwango cha juu cha uchafuzi wa hewa. Inadhuru afya na maisha ya binadamu, inapunguza thamani ya maisha yao, na inaweza kuathiri vibaya uchumi. Athari hizi pia huathiri zaidi watu na jamii zilizo na uwezo mkubwa wa kuathiriwa. Hivi majuzi, katika mwezi wa Juni mwaka wa 2023, New York ilikabiliwa na uchafuzi mbaya zaidi wa hewa uliosababishwa na mioto ya misituni eneo la Amerika Kaskazini ( New York Orange Sky na Burning Eyes).

Uchafuzi wa hewa ndio hatari kubwa zaidi ya kimazingira inayokabili afya ya umma duniani. Uchafuzi wa hewa huwaathiri watu kila mahali; kazini, safarini na majumbani. Kukumbana na uchafuzi wa hewa kupitia kwa chembechembe ndogondogo nyumbani na nje husababisha kwa makadirio vifo milioni 7 vya mapema kila mwaka , kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), na ndiyo sababu kubwa ya ulemavu kwa wale wanaoishi na magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa hewa.

Uchafuzi wa hewa ni tatizo ambalo linaweza kusuluhishwa na mataifa tajiri zaidi yameimarisha sana ubora wa hewa yao katika miongo ya hivi karibuni. Lakini uchafuzi wa hewa sasa unaathiri watu katika nchi zenye chumi za kiwango cha chini na za kiwango wastani kwa kiwango kinachotofautiana.

Katika nchi nyingi zinazokua, kutegemea kuni na fueli mangozinginezo, kama vile makaa kwa ajili ya kupikia na kuota moto, na matumizi ya mafuta ya taa kupata mwangaza, huongeza uchafuzi wa hewa nyumbani, ikidhuru afya ya wanaokumbana na hali hiyo. Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu bilioni 2.7 wanategemea aina hii ya fueli. Nyingi ya athari hizo huathiri pakubwa katika sehemu za Asia na nchi za Afrika zilizo Kusini ya jangwa la Sahara, ambapo ni kawaida kufukiza moshi wakati wa kupika.

Ingawa athari yake kwa afya ya wanadamu ndilo suala sugu, uchafuzi wa hewa pia huathiri sana aina mbalimbali za mifumo ya ikolojia na kupunguza mazao ya mimea na kuathiri misitu. Kadhalika, inapunguza mwonekano wa anga na huongeza uharibifu wa vifaa, majengo, sanamu za makumbusho na maeneo ya urithi wa kitamaduni, na husababisha sehemu nyeti ya mifumo ya ekolojia ya maziwa kuwa na asidi.

Athari hizi za kiafya na mazingira zinahitaji kupunguzwa kwa faida ua vitu hivi. Lakini uchafuzi wa hewa pia unagharimu mno uchumi kwa kuathiri afya ya wanadamu, kupunguza uwezo wa kufanya kazi, kupunguza mazao ya mimea na kupungua kwa ushindani katika miji iliyoungana ulimwenguni. Kwa mfano, gharama ya kimataifa ya kimatibabu katika mwaka wa 2016 pekee kutokana na uchafuzi wa hewa ya nje ilikadiriwa kuwa US$ trilioni 5.7 , sawa na asilimia 4.8 ya Jumla ya Pato la Taifa katika mwaka huo.

Kadhalika, uchafuzi wa hewa unahusishwa sana na mabadiliko ya tabianchi, na gesi nyingi za ukaa (GHGs) na uchafuzi wa hewa kutoka vyanzo sawa. Vichafuzi vingi vya hewa huathiri vibaya afya ya wanadamu na hali ya hewa , na hivyo kuathiri maisha ya watu leo na kufanya siku zijazo kutokuwa salama kwa vizazi vijavyo. Hatua zilizoratibiwa za kupunguza uchafuzi wa hewa na GHGs, kama vile zile zinazoshughulikia Uchafuzi wa Hali ya Hewa wa Muda Mfupi (SLCPs), zinaweza kusababisha manufa makubwa mno afya ya umma na kwa mazingira.

Uhusiano kati ya uchafuzi wa hewa na ustawi, uchumi na mazingira kunamaanisha kwamba kupunguza uchafuzi wa hewa kunahusiana na kufanikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) , na kunaathiri moja kwa moja kufanikiwa kwa SDG 3: Afya Bora na Hali njema , SDG 7: Nishati ya Bei Nafuu na Isiyochafua Mazingira, SDG 11: Miji na Jamii Endelevu , na SDG 13: Mabadiliko ya Tabianchi. Inaathiri SDGs nyingi nyinginezo kwa njia ilsiyokuwa ya moja kwa moja.

Uchafuzi wa hewa pia umehusishwa na janga tandavu la sasa la COVID-19. Uchunguzi uliofanywa katika miezi ya kwanza ya janga hilo ulionyesha uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vya uchafuzi wa hewa na kuongezeka kwa uwezekano wa kushambuliwa na ugonjwa huo. Utafiti pia ulisema kwamba kuenea kwa janga tandavu la COVID-19 huenda kunasaidiwa na uchafuzi wa hewa. Tafiti hizo zinahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi lakini pia zinatoa sababu nyingine ya kuchukua hatua dhidi ya uchafuzi wa hewa.

Kutokana na yaliyotendeka zamani na sasa, tunajua kwamba uchafuzi wa hewa unaweza kuepukwa, na kama mifano inavyoonyesha, kupunguza uchafuzi wa hewa kutakuwa na manufaa zaidi kama vike kuwa na afya bora na kuwa na uwezo wa kufanya kazi zaidi, kuwa na mazingira bora zaidi, kupunguza umasikini na kuongezeka kwa mafanikio.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Ukweli muhimu kuhusu uchafuzi wa hewa ya nje na vyanzo vikuu vya uchafuzi (WHO)
  2. Uchafuzi wa Hali ya Hewa wa Muda Mfupi na athari zake kwa afya, hali ya hewa, na kilimo (CCAC)
  3. Athari za uchafuzi wa hewa (OECD)
  4. Nishati na Uchafuzi wa Hewa (IEA)
  5. Video: Michakato ya uchafuzi wa hewa na athari yake (WMO)
  6. Video: Uhusiano kati ya ubora wa hewa na hali hali ya hewa (WMO)

 

  1. UCHAFUZI WA HEWA NI NINI?

Uchafuzi wa hewa husababishwa na gesi na chembechembe zinazoruhusiwa kuingia angani kupitia shughuli mbalimbali za kibinadamu, kama vile mwako usiotosha wa fueli, kilimo, na ukulima. Pia kuna vyanzo vya asili vinavyochangia uchafuzi wa hewa, ikiwa ni pamoja na chembechembe za vumbi la mchanga na chumvi kwenye bahari.

Uchafuzi wa hewa unaweza kutoka moja kwa moja kutoka kwa chanzo (kwa mfano, uchafuzi wa kimsingi) au unaweza kutokana na athari za kemikali kwenye anga (kwa mfano, uchafuzi wa pili). Wakati uchafuzi huu unakolea na kufikia viwango hatari kwenye hewa, huwadhuru wanadamu, wanyama, mimea na mifumo ya ikolojia, unapunguza uwezo wa kuona na kuharibu vifaa, majengo na maeneo ya urithi wa kitamaduni.

Vyanzo vikuu vya uchafuzi vinavyoathiri afya ya binadamu ni chembechembe ndogo , ozoni ya kiwango cha chini (O 3 ) na { 6> nitrojeni dioksidi (NO2) . Chembechembe ndogo zinazodhuru afya ya binadamu zinazojulikana kama PM2.5 (chembe zenye kipenyo cha chini ya mikromita 2.5), ambazo zinaweza kuingia ndani kabisa kwenye mapafu na kupita kwenye mfumo wa damu na kuathiri viungo tofautitofauti na kazi za mwili. Chembechembe hizi zinaweza kutolewa moja kwa moja au kutengenezwa angani kutokana na vyanzo vingi tofauti tofauti vya uchafuzi (kwa mfano amonia (NH 3 ) , na mchanganyiko wa mvuke wa ogani (VOCs) ).

Ozoni (O₃), ni chanzo cha uchafuzi wa daraja la pili. Inaweza kusababisha mapafu kuwasha sana na kuzuia mimea kurefuka. Kadhalika ni gesi mbaya mno ya ukaa (GHG). O₃ inatengenezwa kwenye sehemu ya chini ya anga (troposphere), karibu na sehemu ya Dunia, kutona na athari zinazotokea vichafuzi fulani vikikumbana na mwanga wa jua. GHG yenye nguvu, methani (CH₄), ndicho chanzo kikubwa cha kutengenezwa kwa O₃ Ozoni hii ya sehemu ya chini ya anga ni tofauti na ozoni iliyo kwenye sehemu ya juu zaidi ya anga (stratosphere), inayotukinga kutokana na miale hatari ya jua.

Nitrojeni Oksidi (NOx) ni mkusanyiko wa aina mbalimbali ya kemikali zinazochafua hewa, zinazojumuisha nitrojeni dioksidi (NO2) na nitrojeni monoksidi (NO). NO2 ndio hatari zaidi kati ya michanganyiko hii na hutokana na shughuli zinazoendeshwa na mwanadamu. Inathiri afya ya binadamu, inapunguza mwangaza angani, na inaweza kuchangia pakubwa katika mabadiliko ya tabianchi, katika viwango vya juu. Mwishowe, ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa O₃.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Maelezo ya jumla ya uchafuzi wa hewa na athari zake (WHO)
  2. Uchafuzi wa Hali ya Hewa wa Muda Mfupi na athari zake kwa afya, hali ya hewa, na kilimo (CCAC)
  3. Maelezo ya jumla ya Nitrojeni Dioksidi (NO2 ) (US EPA)
  4. Uchafuzi wa Chembechembe Ndogondogo (PM) ni nini (US EPA)

 

  1. JE, UCHAFUZI WA HEWA UMEKUWA CHANGAMOTO KWA KIPINDI GANI?

Uchafuzi wa hewa umehusishwa na wanadamu kwa maelfu ya miaka, kuanzia na matumizi ya moto kwa kupikia na kuota moto. Viwango hatari vya uchafuzi wa hewa ya nje vilikuja kuwa tatizo wakati wa mapinduzi ya viwanda, ambapo utumiaji wa makaa ya mawe ulisababisha uchafuzi mkubwa wa hewa mijini.

Kisa cha ukungu ya London mnamo mwaka wa 1952, ni mfano mkuu, uliosababisha ongezeko katika idadi ya vifo kwa kipindi cha juma moja. Uchafuzi kutoka kwa moto wa makaa ya mawe katika sehemu za makazi, makaa ya mawe kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, matumizi ya mafuta machafu kwa ajili ya usafirishaji, na uchafuzi wa mazingira ya viwandani, uliingiliana na hali ya hewa ambayo ilisababisha uchafuzi wa mazingira ya London na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 12,000 kwa siku hizi chache. Kilio cha umma kilichofuata, kilisababisha kupitishwa kwa Sheria ya Hewa Safi ya Uingereza (1956). Vipindi vingine vya uchafuzi wa hewa wenye madhara makubwa, k.m. katika Donora, USA (1948), na Meuse Valley, Ubelgiji (1930), kulichochea hatua kama hizo kuchukuliwa ili kukabiliana na uchafuzi wa hewa katika nchi nyingine.

Kuendelea kutegemea mafuta ya visukuku hadi karne ya 20 kulisababisha uchafuzi wa hewa kuongezeka kadiri nchi zinavyoendela kiviwanda. Katika nchi zenye maendeleo mapya ya viwanda kama Uchina na India, hili limesababisha hali mbaya ya uchafuzi wa hewa, kama ilivyoshuhudiwa awali huko Marekani na Ulaya. Hata hivyo, aina mpya za nishati jadidifu isiyochafua mazingira, na kupitishwa kwa kanuni za ubora wa hewa na michakato ya usimamizi, zinapunguza utegemeaji wa baadhi ya fueli na mazoea yenye kuchafua. Beijing, iliyowahi kujulikana kwa shida yake ya uchafuzi wa hewa, kwa miaka 20 iliyopita imechukua hatua kali ili kupunguza uchafuzi wa hewa na ubora wake wa hewa umeimarika sana.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Maelezo ya jumla ya uchafuzi wa hewa na athari zake (WHO)
  2. Historia ya uchafuzi wa hewa (US EPA)
  3. Ripoti: “Ukaguzi wa Udhibiti wa Uchafuzi wa Hewa wa Miaka 20 huko Beijing” (UNEP)

 

  1. UCHAFUZI WA HEWA UNATOKA WAPI?

Uchafuzi wa hewa hutokana na vyanzo vingi mbalimbali , vya asili na vya mwanadamu (anthropogenic). Vyanzo vya asili ni pamoja na milipuko ya volkeno, mnyunyizo wa bahari, vumbi la mchanga, moto wa mimea ya asili na radi. Baadhi ya vyanzo vya kawaida vinavyotokana na shughuli za binadamu ni pamoja na uzalishaji wa umeme, uchukuzi, viwanda, kupika na kupasha joto nyumbani, kilimo, kutumia viyeyushi, mafuta na uzalishaji wa gesi, kuchoma taka na ujenzi. Vyanzo vingine, kama vile moto wa misitu na savanna, na vumbi la madini linalopeperushwa, hujitokeza kiasili, lakini huzidishwa na shughuli za wanadamu.

Kwa idadi kubwa ya watu ulimwenguni, shughuli za wanadamu huchangia pakubwa uchafuzi wa hewa ambao wanaona.

Uchafuzi tofautitofauti una vyanzo tofautitofauti. Katika miji, uchafuzi wa hewa hutoka ndani na nje ya mipaka ya jiji, baadhi yake husafiri umbali mrefu. Vyanzo vikuu vya uchafuzi mijini ni pamoja na magari, kuchoma gesi, makaa ya mawe na makaa, kuni za kupikia na kupasha joto, na kutoka kwa viwanda vinavyopatikana mijini. Vyanzo vingi vikubwa vya uchafuzi viwandani, kama vile viwanda vya saruji, viwanda vya chuma na vya uzalishaji wa umeme, vinapatikana mbali na miji, lakini bado huchangia sana kwa viwango vya mijini, kwa sababu ya husafirishwa na hewa kwa umbali mrefu. Uchafuzi unaotokana na viwanda vya mafuta na gesi na sekta ya bahari pia unaweza kusafiri kwa umbali mrefu sana.

Uchafuzi unaotokana na kilimo, ikiwa ni pamoja na kuchoma ili kuandaa eneo la kilimo, na moto wa misitu, vinachangia pakubwa katika viwango vya uchafuzi wa hewa wa mijini na vijijini. Katika maeneo ya kiangazi, karibu na majangwa na ardhi iliyomomonyoka, vumbi linalopigwa na upepo linaweza kuchangia sehemu kubwa ya PM2.5. Amonia nyingi hutokana na kilimo na ushughulikiaji wa kinyesi cha binadamu.

Mojawapo ya vyanzo vikuu vya uchafuzi wa hewa katika maeneo ya vijijini na vijiji vilivyo karibu na miji katika nchi zenye kipato cha chini, hutoka kwa nyumba zinachoma majani, fueli mango (k.m. makaa ya mawe) au mafuta ya taa kwa kupikia, kupasha joto na kutoa mwangaza. Uchafuzi wa hewa nyumbani pia huchangia uchafuzi wa hewa ya nje.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Uchafuzi wa hewa ya nje (WHO)
  2. Uchafuzi wa hewa ya ndani ya nyumba (WHO)
  3. Ukweli muhimu kuhusu uchafuzi wa hewa ya nje na vyanzo vikuu vya uchafuzi (WHO)
  4. Vyanzo vya uchafuzi wa hewa Ulaya (EEA)
  5. Makadirio ya WHO ya mfichuo wa uchafuzi wa hewa kwa nchi na athari za kiafya

 

  1. JE, UCHAFUZI WA HEWA NI TATIZO LA KARIBU TU AU LINAWEZA KUSAFIRI MWENDO WA MBALI?

Uchafuzi wa hewa huathiri sana maeneo yaliyo karibu na chanzo chake, lakini kwa sababu unaweza kusafirishwa umbali mrefu angani, uchafuzi wa hewa ulioanzia katika sehemu moja, unaweza pia kuathiri maeneo ya mbali. Kwa mfano, vyanzo vya uchafuzi ambavyo hugeuka kuwa chembechembe ndogondogo (PM 2.5) na ozoni (O3) vinaweza kusafiri kwa zaidi ya mamia au maelfu ya kilomita, ikisababisha athari za kikanda na za bara. Uchafuzi huu wa hewa unaopita mipaka unasababisha changamoto katika masharti na utekelezaji kwa sababu nchi au mikoa mbalimbali, ina udhibiti mdogo kuhusu uchafuzi wa hewa unaokuja kutoka nje ya mipaka yao (Pia tazama swali la 14).

Licha ya mchango wa vyanzo vya uchafuzi wa hewa vilivyo mbali kwa uchafuzi wa hewa wa mahali hapo, vyanzo vilivyo karibu vinabaki kuwa visababishi vikuu vya ubora wa hewa ya mahali hapo. Vyanzo vya uchafuzi kama nitrojeni dioksidi (NO2) na salfa dioksidi (SO2), vina viwango vya ukolezi ambavyo viko juu sana vikiwa karibu na vyanzo vyake (usafirishaji, uzalishaji wa nishati na viwanda). Ndani ya jiji, maeneo yaliyo karibu na vyanzo vikubwa yanaweza kuwa na viwango vikubwa vya uchafuzi, ilhali maeneo mengine ya jiji hilo yanaweza kuwa safi zaidi.

Hali ya anga kama vile upepo, huathiri mtawanyiko wa uchafu na inaweza kutofautiana sana. Upepo mkali unawezesha usafirishaji wa umbali mrefu, na hali zilizotulia zinaweza kusababisha kuongezeka kwa vyanzo vya uchafuzi. Miji mikubwa katika mikoa inayokaribia tropiki na ya kitropiki ambayo ina upepo hafifu na saa nyingi za jua, hupata matukio mabaya ya uchafuzi wa mazingira. Milima inayozunguka miji, hewa ya bahari na hali nyingine za hewa zinaweza kuathiri kuenea kwa uchafuzi na kuathiri kutengenezwa kwa vyanzo vya uchafuzi vya kisekondari.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Mkutano wa Uchafuzi wa Hewa wa Umbali Unaopita Mipaka (UNECE)
  2. Kipengele cha afya cha uchafuzi wa hewa wa umbali unaopita mipaka (WHO)
  3. Video: Michakato ya uchafuzi wa hewa na athari (WMO)

 

  1. NI NINI ATHARI YA UCHAFUZI WA HEWA KWA AFYA YA BINADAMU?

Chanzo cha uchafuzi wa hewa kinachotishia sana afya ya binadamu ni chembechembe ndogo. Kina kipenyo cha mikromita 2.5 au kidogo, inayojulikana pia kama PM2.5. Chembechembe hizi ndogo hazionekani kwa jicho la mwanadamu na ni mara 40 ndogo kuliko upana wa unywele wa mwanadamu. Zinaweza kusababisha uharibifu mkubwa katika miili yetu. Chembechembe hizi ni ndogo vya kutosha ili kupenya hadi ndani ya mapafu yetu, ambapo husababisha kuvimba kwa tishu nyeti za mapafu na zinaweza kupita kwenye mfumo wa damu, na kuathiri viungo kama moyo na ubongo. WHO inakadiria kuwa mfichuo wa PM2.5 husababisha vifo milioni 7 vya mapema kila mwaka .

Uchafuzi wa hewa husababisha magonjwa mabaya na sugu. Kuna uthibitisho mkubwa unaohusisha kukumbana kwa muda mrefu kwa uchafuzi wa hewa na na kuwa na uwezekana mkubwa wa kupatwana ugonjwa wa moyo wa ischaemic, kiharusi, ugonjwa sugu wa mapafu (COPD), saratani ya mapafu na inayoathiri mfumo wa kusiaga chakula, na kuathiri vibaya ujauzito (yaani, uwezo mdogo wa kuzaa, kuzaa kabla ya wakati na kupunguzwa kwa uzito wa mtoto anapozaliwa (watoto wanapozaliwa wakiwa na uzito wa chini ya pauni tano), ugonjwa wa sukari na mtoto jichoni. Wakala wa Kimataifa wa Utafiti wa Saratani ya WHO (IRCA) , imeanisha uchafuzi wa hewa kama kisababishi cha kansa .

Baadhi ya athari za kiafya za moja kwa moja za uchafuzi wa hewa zinajumuisha kuwashwa kwa macho, pua na koo, matatizo ya kupumua, kikohozi, na kuzidisha hali zilizokuwepo kuwa mbaya zaidi, kama pumu, na maumivu ya kifua. Umri, magonjwa yaliyokuwepo awali, hatari zingine za ugonjwa hurahisisha kuathiriwa na uchafuzi, zinaweza kuathiri jinsi mtu anavyoshughulikia chanzo cha uchafuzi.

Gesi zinazochafua hewa pia zinaweza kuwa hatari sana. Kaboni monoksidi (CO), huzuia usafirishaji wa oksijeni kwa tishu na inaweza kusababisha kifo ikiwa kwa viwango vya juu sana. Salfa dioksidi (SO2), husababisha kuwashwa kwa mapafu na hivyo kuathiri afya ya wale walio na ugonjwa unaoathiri mfumo wa kupumulia (pumu na COPD), hasa wale wanaoishi na kufanya kazi karibu na vyanzo vya SO2. Nitrojeni oksidi (NOx) zinahusishwa na athari nyingi, kuanzia kuwashwa na mfumo wa kupumulia, hadi kupata ugonjwa wa pumu na ongezeko la vifo. Kukumbana na ozoni (O 3) husababisha magonjwa ya kupumua na ulihusishwa na vifo 472,000 vya mapema mnamo 2017, kulingana na Mzigo wa Ugonjwa Ulimwenguni (IHME).

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Ripoti: Athari za kiafya za uchafuzi wa hewa (Taasisi ya Athari za Afya)
  2. Athari za kiafya za hewa ya mazingira (WHO)
  3. Utangulizi kwa uchafuzi wa hewa ya mazingira (nje) (WHO)
  4. Ripoti: Uchafuzi wa hewa na Saratani (WHO) (WHO)

 

  1. JE, KUNA VIWANGO VYOVYOTE VINAVYOKUBALIKA VYA UCHAFUZI WA HEWA KWA AFYA: NJE AU NDANI YA NYUMBA?

Ingawa watu wote huathiriwa kwa njia tofautitofauti kiafya kutokana na uchafuzi wa hewa, katika miji mikubwa au watu nchini kwa ujumla, hakuna ushahidi wa kiwango salama kabisa cha uchafuzi wa hewa, hasa kuhusiana na chembechembe ndogo. Hata hivyo, ili kusaidia nchi kufikia hewa safi kwa afya, WHO imeweka kanuni za viwango vya kawaida kwa vyanzo vikuu vya uchafuzi wa hewa, ambayo zaidi yake, athari mbaya kwa afya za watu zinawezeka kutokea. Kwa mfano, WHO inakadiria kwamba kupunguza kiwango cha wastani cha mwaka cha chembechembe ndogondogo (PM2.5 ) kutoka kiwango cha mikrogramu 35 mchemraba (μg/m3), (mwongozo wa mpito wa ubora wa hewa inayotumika sana katika miji mingi ya nchi zinazokua), kwa mwongozo wa kiwango cha WHO cha 10 μg/m3, kunaweza kupunguza vifo vinavyosababishwa na uchafuzi wa hewa kwa asilimia15.

Hii haimaanishi kwamba hakuna athari za kiafya ndani ya miongozo hiyo, lakini inawakilisha malengo ya msingi ya kiafya inayosaidia kufuatilia athari za magonjwa yanayotokana na uchafuzi wa hewa, na kutaja malengo na viwango vya kitaifa, na kuchunguza ufanisi wa juhudi za usimamizi wa ubora wa hewa zilizowekwa ili kuboresha afya.

Nchi nyingi zimeweka viwango vya ubora wa hewa ya kitaifa. Viwango vya kitaifa vinaweza kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine na vinaweza kuwa juu au chini ya viwango vilivyowekwa na WHO. Ni suala la sera kuamua ni vikundi vipi hususan vilivyo hatarini vinavyopaswa kulindwa na viwango, na ni kiwango gani cha hatari kinakubalika. Hata hivyo, nchi nyingi zinajitahidi kufikia vigezo vya ubora wa hewa vya WHO na malengo yake ya mpito.

Mkataba wa UNECE kuhusu Uchafuzi wa hewa wa umbali mrefu unaopita mipaka pia umetoa viwango (vikuu) vya ozoni (O3) , ambavyo vikizidi, vinaweza kuathiri mimea na uoto wa asili.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Miongozo ya Uboreshaji wa Hewa ya WHO (WHO)
  2. Ripoti: Ripoti ya Hali ya Hewa Duniani ya mwaka wa 2019 (IHME)
  3. Itifaki ya Kupunguza Asidi, Kuongeza Virutubishi na Kiwango cha chini cha Ozone (UNECE)
  4. Athari zenye Kufisha za Vipande vya Chembe kwenye Hewa
  5. Kituo cha Uratibu wa Athari (LRTAP)

 

  1. JE, UCHAFUZI WA HEWA UNA ATHARI GANI KWA CHAKULA, MIMEA, MISITU NA BAYOANUAI?

Ozoni (O3) ndicho chanzo kikuu zaidi cha uchafuzi wa hewa unaoathiri ukuzi wa mimea. Inapunguza mazao ya vyakula, ubora wa misitu na bayoanuai kwa ujumla. Spishi mbalimbali za mimea huathiriwa kwa njia tofauti na 03; zile zinazoathiriwa sana na O3 zitapungukiwa na uwezo wa kushindana katika mifumo ya ikolojia, huku spishi sugu zikitawala. Mimea mingine huathiriwa sana na O3, hasa maharagwe. Mazao ya soya, kwa mfano, yanaweza kupunguzwa kwa asilimia 15 au zaidi. Kadhalika, kuna athari ya moja kwa moja kwa hali ya hewa, wakati ukuzi wa miti ya misitu unapopungua kwa sababu ya uchafuzi wa O3 , unapunguza uwezo wa misitu kufyonza kaboni dioksidi na uwezo wake wa kusaidia kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa.

Vyanzo vingine vya uchafuzi kama salfa na nitrojeni pia vinaweza kudhuru mifumo ya ikolojia ya misitu na maziwa, kupitia asidi ya mchanga na uso wa maji, ikiathiri ukuzi wa msitu na kuua samaki na viumbe vingine. Utoaji wa nitrojeni pia husababisha kuongezeka kwa virutubishi (kupitia mbolea) kwa mifumo ya ikolojia iliyo na virutubishi vichache kama vile maeneo ya joto, ikisababisha mabadiliko makubwa kwa bayoanuai.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Uchafuzi wa hewa, mifumo ya ikolojia na viumbe hai (UNECE)
  2. Ripoti: Utathmini wa Athari za Uchafuzi wa Hewa kwa Huduma za Mifumo ya Ikolojia - Kujaza Pengo na Mapendekezo ya Utafiti (Defra)
  3. Makala: Athari za Uchafuzi wa Hewa kwa Mazingira na Afya: Ukaguzi (Manisalidis I., et al. 2020)
  4. Athari za Uchafuzi Hewa kwa Mimea ya Kilimo (OMAGFRA)

 

  1. JE, UCHAFUZI WA HEWA HUSABABISHA UHARIBIFU MWINGINE WA MAZINGIRA?

Baadhi ya vyanzo vya uchafuzi wa hewa husababisha 'mvua ya asidi,’ tatizo lililozingatiwa kwa njia ya kipekee Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika miaka ya 1980 na 90. Salfa dioksidi (SO2) na nitrojeni oksidi (NOx) huchanganyika na maji angani, na kuunda asidi ya salfa na asidi ya nitriki ambayo hurudi duniani kama ‘mvua ya asidi'.

Mvua ya asidi huathiri mazingira kwa kuharibu majani ya mimea, na hivyo kupunguza uzalishaji wa mmea, na inaweza kuondoa virutubishi vilivyo kwenye udongo vinavyohitajiwa na mimea ili kuishi. Ardhi na maji ya mito inapokuwa na asidi inaweza kuua samaki na wadudu, na kuathiri spishi nyingine ambazo huzitegemea kwa chakula. Mvua ya asidi pia inajulikana kusababisha uharibifu wa majengo na sanamu za ukumbusho.

Mvua ya asidi huko Ulaya na Amerika ya Kaskazini imepungua sana kwa sababu ya udhibiti mkali wa uzalishaji wa SO2 na NOx, kama vile U.S. Sheria ya Hewa Safi ya 1970 , Mkataba wa Ubora wa Hewa mnamo 1991 wa Canada na Marekani, na hatua kama hizo Ulaya. Ingawa mvua ya asidi imepungua huko Ulaya na Amerika ya Kaskazini, imesalia kuwa tishio huko Asia.

Erosoli na kemikali zilizo na oksidi (k.v ozoni) pia zinaweza kutengeneza ukungu na kupunguza uwezo wa kuona, ambao unaweza kugubia miji kwa ukungu na moshi. Viwango vinavyopungua huko Amerika ya Kaskazini na Ulaya vimepunguza ukungu huu kwa kiasi kikubwa, lakini vinaenea sana katika sehemu nyingine za ulimwengu, hasa Asia. Uhusiano mkubwa kati ya mwonekano na uchafuzi wa mazingira ulionyeshwa wakati watu katika sehemu za Kaskazini mwa India waliweza kuona Himalaya kwa mara ya kwanza katika kizazi, wakati viwango vya uchafuzi wa hewa vilipungua kwa sababu ya vizuizi vya kutoka nje na kupungua kwa uchafuzi, uliosababishwa na janga tandavu la COVID-19.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Mvua ya Asidi ni nini? (USEPA)
  2. Habari ya Msingi Kuhusu Mwonekano (USEPA)
  3. Mvua ya Asidi na Maji (USGS)

 

  1. NITAJUAJE KIWANGO CHA TATIZO LA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KATIKA NCHI YANGU/JAMII?

Miji mingi imetekeleza mitandao ya ufuatiliaji ambayo inaendelea kupima uchafuzi wa hewa kama sehemu ya mifumo yao ya usimamizi wa ubora wa hewa. Wengi wao huripoti kwa ukawaida Kiashiria cha Ubora wa Hewa (AQI) ambacho ni rahisi kuelewa, na mara nyingi hutiwa rangi, kuonya kuhusu viwango hatari vya uchafuzi wa hewa. Taarifa hiyo inapatikana kupitia Wavuti, magazeti na programu za kiteknolojia. Nchi zinafafanua fahirisi zao kulingana na viwango vyao vya ubora wa hewa. Kwa hivyo, haziwezi kulinganishwa kati ya nchi na zimeundwa kwa madhumuni ya habari ya umma.

Kupatikana kwa ufuatiliaji wa ubora wa hewa hakulingani ulimwenguni na katika mikoa. Hii ni kwa sababu vifaa vya kufuatilia vya hali ya juu ni ghali, kama tu jinsi ilivyo gharama ya kuwazoeza watu kuvitumia na kudumisha mitandao hiyo. Hata katika sehemu zenye ufuatiliaji mzuri, kasoro hupatikana. Kwa mfano, katika baadhi ya sehemu za Ulaya , kuna mitandao mingi sana ya ufuatiliaji, ilhali katika sehemu nyingine, mitandao si mingi sana. Katika nchi nyingi zinazostawi ulimwenguni hakuna vifaa rasmi vya ufuatiaji wa uchafuzi wa hewa.

Kuwekeza katika vipimo vya ufuatiliaji wa ubora wa hewa ni muhimu sana kwa sababu kadiri mitandao inavyokuwa mikubwa ndivyo tunavyoweza kuwa na habari nyingi zaidi kwa ajili ya jiji, eneo au nchi. Taarifa hii inaweza kuwa yenye thamani sana katika kuwasaidia watu waelewe viwango vya uchafuzi wa hewa katika eneo wanaloishi na hatua za kuchukua ili kujipunguzia hatari. Kadhalika, ni muhimu kwa serikali, kuweza kufanya maamuzi kuhusu mipango ya muda mfupi na muda mrefu ili kupunguza uchafuzi wa hewa.

Katika maeneo mengi kampuni za kibinafsi zinafanyiza vifaa vya gharama ya chini vya kufuatilia ubora wa hewa ambavyo watu wanaweza kuweka nyumbani mwao. Jambo hili linawezesha kuwepo kwa mitandao ya raia wanasayansi kuripoti kuhusu ubora wa hewa na mifumo ya data ya ubora wa hewa mitandaoni inayoongozwa na raia.

Idadi kubwa ya mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia, na kampuni za kibinafsi pia hukusanya na kuripoti habari kuhusu ubora wa hewa, mara nyingi kwa kutegemea kujumlisha data ya vifaa vya kufuatilia na setilaiti. Mahali ambapo habari za eneo hususa hazipatikani, hizi zinaweza kuwa rasmali muhimu zinazosaidia kuelewa tatizo la uchafuzi wa hewa katika jiji au nchi yako.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Mfumo wa Habari wa Ulimwenguni Kote wa Uchafuzi wa Hewa ya Nje Katika Miji wa WHO
  2. BreatheLife – kampeni ya Ulimwenguni Kote ya hewa safi
  3. Tatizo la Ulimwenguni Kote la Ugonjwa (IHME)
  4. Habari kuhusu ubora wa hewa (Huduma za Kufuatilia Anga Hewa)
  5. Hali ya Wavuti ya Hewa ya Ulimwenguni Kote
  6. Wavuti ya Kupumua ya London (Breathelife)
  7. Uchafuzi wa Hewa wa Beijing: Kipimo cha Wakati Hususa cha Ubora wa Hewa (AQI)

 

  1. JE, UCHAFUZI WA HALI YA HEWA UMETATULIWA KOKOTE?

Uchafuzi wa hali ya hewa haujatatuliwa katika eneo lolote, lakini kumekuwa na upungufu mkubwa wa hewa chafu inayotolewa na viwango vikubwa vya vyanzo vya uchafuzi katika nchi nyingi za Ulaya, pamoja na Marekani, Kanada na Japani, ambapo sera zenye nguvu, sheria na mifumo ya kufuatilia ya kawaida iliwekwa.

Mojawapo ya mifano inayojulikana sana ni London, ambayo ilikuwa na baadhi ya viwango vibaya zaidi vya uchafuzi, kabla ya majiji mengine, ambayo huenda ilifikia kilele mwaka 1900. Tangu wakati huo, ubora wa hewa huko UK umeboreka sana. Viwango vya uchafuzi wa hewa vimeteremka kwa zaidi ya asilimia 97% kati ya mwaka wa 1900 na 2016. Majiji na maeneo mengine pia yameonyesha upungufu mkubwa, uliotokana na sera kama hizo. Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba uchafuzi wa hewa umetatuliwa. Huko London– PM 2.5 ingali juu zaidi kuliko kiwango cha ubora wa hewa cha WHO.

Jiji la Mexico ni mfano mwingine wa jinsi majiji yamepunguza uchafuzi wao wa hewa kwa kiwango kikubwa. Jiji hilo lilikuwa na tatizo kubwa sana la uchafuzi wa ozoni (O₃) katika miaka ya 1980. Kutoka kilele katika mwaka wa 1989, viwango vya O₃ vimepunguka kwa theluthi mbili kufikia 2015 – hata hivyo viwango vingali juu vya kutosha kusababisha madhara makubwa ya kiafya, lakini kivyovyote vile ni upungufu mkubwa.

Upungufu huu unaonyesha kwamba uchafuzi wa hewa ni tatizo tunalojua jinsi ya kusuhulisha, na kwamba kuna sera na teknolojia zinazohitajika ili kupata hewa safi zaidi. Katika nchi nyingi, ubora wa hewa umepatikana huku utajiri wa nchi ukiongezeka. Hilo linaonyesha kwamba tofauti na hapo awali, ambapo uchafuzi wa hewa ulionekana kuwa gharama isiyoepukika ya ukuzi wa kibiashara, upungufu wa uchafuzi wa hewa hauathiri ukuzi wa kibiashara. Haihusiani kikamili na kutengeneza utajiri.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Historia ya kufaulu kwa Sheria ya Marekani ya Hewa Safi katika kupunguza uchafuzi wa hewa kutoka kwa sekta ya usafiri
  2. Makala: Uboreshaji wa Hewa Beijing ni Mfano Kwa Majiji Mengine (UNEP)
  3. Ubora wa hewa: kufafanua uchafuzi wa hewa – kwa kuchunguza kijuu juu (Defra)
  4. Athari za uchafuzi wa hewa (OECD)

 

  1. NI HATUA ZIPI ZINAZOWEZA KUCHUKULIWA NA SERIKALI ILI KUBORESHA HEWA?

Serikali zina wajibu wa kuwaandalia raia zao hewa safi. Kuna machaguo kadhaa kwa serikali ya kitaifa na serikali za eneo ili kuongeza ubora wa hewa. Uchafuzi wa hewa ni tatizo ambalo tunajua jinsi ya kusuluhisha.

Serikali zinahitaji kuekeza katika uwezo wa kupima na kufuatilia uchafuzi wa hewa kwa kuanzisha mitandao ya kufuatilia; na kuhakikisha kwamba mitando hiyo inatumika vizuri, kudumishwa, na kupitishwa kwa utaratibu wa kuhakikisha ubora na kutegemeka kwa vipimo vya ubora wa hewa.

Hatua ya kwanza ya kusimamia vizuri uchafuzi wa hewa ni kuhakikisha kuwa sheria zinazohitajika, sera na mifumo ya utekelezaji ipo na inategemezwa vizuri. Serikali zinapaswa kuhakikisha kuwa taasisi zinazofaa zina uwezo wa kufuatilia na kutathmini uchafuzi wa hewa. Hili litahakikisha kwamba wanaofanya maamuzi wanajua uchafuzi wa hewa unatokea wapi, ukubwa wa vyanzo mbalimbali vya uchafuzi na viwango vya uchafuzi katika maeneo tofauti ya nchi yao, athari za kiafya, na ni hatua gani zenye matokeo makubwa zinazoweza kuchukuliwa kupunguza viwango vya uchafuzi na madhara yanayotokezwa.

Iwapo uwezo wa kuchukua hatua hizo ni mdogo au hakuna habari za eneo hilo, bado kuna raslimali zinazoweza kupatikana ili kusaidia nchi kuelewa tatizo lao la uchafuzi wa hewa na kutambua hatua zinazoweza kutangulizwa. Hizi ni pamoja na vyanzo vya uchafuzi, vilivyokadiriwa na programu za ulimwenguni kote (k.m. makadirio ya uchafuzi ya EDGAR [NB1] ), au viwango vya juu na matokeo kwa afya (WHO, IHME, Hali ya Hewa ya Ulimwenguni Kote ), iliyokadiriwa kutoka setilaiti na kielelezo cha ulimwenguni Kote, na kusema kweli katika vituo vya ufuatiliaji. Vikundi hivi vya takwimu vina upungufu wake na mambo yasiyotarajiwa na vinapaswa kutumiwa katika visa ambapo habari za eneo hususan hazipatikani, au mahali ambapo kuna uwezo mdogo wa ufuatiliaji.

Ni muhimu kwa serikali kuelewa faida na gharama zinazohusika katika hatua mbadala au njia za kuboresha hewa; na kutanguliza hatua. Nyingi kati ya hatua za kupunguza uchafuzi wa hewa zina faida za kiafya na kijamii ambazo zinazidi kwa kiwango kikubwa gharama za kuzitekeleza.

Mambo makuu ya kufaulu yanatia ndani kuimarisha taasisi na usimamizi, kuchochea mabadiliko ya tabia, kusisitiza utamaduni wa hewa safi, kuimarisha uwezo wa sekta zote, kushiriki na kuchangia suluhisho, kujitolea kisiasa, na kuongeza ufadhili.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Ripoti: LMIC Suluhisho la Uchafuzi wa Hewa Mijini (USAID)
  2. Ripoti: Suala la wajibu wa haki za kibinadamu linahusiana na kufurahia mazingira yaliyo salama, safi, mazuri na yanayoweza kudumishwa (UN)
  3. Mwongozo wa Uchafuzi wa Hali ya Hewa wa London: Muhtasari (Hewa ya London)
  4. Chunguza takwimu: Uchafuzi wa hewa na afya (Hali ya Hewa Ulimwenguni)

 

  1. KWA NINI USHIRIKIANO WA KIENEO NI MUHIMU KATIKA KUSHUGHULIKIA UCHAFUZI WA HEWA?

Kwa kuwa baadhi ya vyanzo vya uchafuzi wa hewa husafiri mwendo mrefu na kuvuka mipaka, mbinu inayoshirikisha nchi kadhaa au eneo fulani ni muhimu ili kushughulikia uchafuzi wa hewa unaokithiri mipaka. Ushirikiano wa kimataifa huwezesha kubadilishana ujuzi wa mambo waliyopitia na mazoea mazuri, na huboresha mtazamo na raslimali zinazohitajika ili kushughulikia tatizo la uchafuzi wa hali ya hewa kwa kiwango kinacholingana na ukubwa wa tatizo.

Mfano mzuri wa mambo chanya yaliyotimizwa na muungano wa serikali za mataifa mbalimbali katika mfikio wa kupunguza uchafuzi wa hewa ni UNECE Kusanyiko kuhusu Uchafuzi wa Hewa Ulioenea Sana na Unaokithiri Mipaka , ambalo lilikuwa mfikio wa kwanza ulioratibiwa kati ya nchi ili kushughulikia matatizo ya uchafuzi wa hewa ya kawaida na yanayofanana. Kadhalika, ushirikiano wa kisayansi umeanzishwa katika Asia, na Mtandao wa Mashariki mwa Asia wa Kufuatilia Utupaji wa Asidi (EANET) ambao umekuwa ukijenga uwezo na ushirikiano katika kufuatilia kati ya Mashariki na Kusini Mashariki mwa Asia. Makubaliano ya Ushirika wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia ya Uchafuzi wa Haze Unaozidi Mipaka (ASEAN) umeanzishwa ili kupunguza uchafuzi wa hewa unaotokana na mioto ya misitu ya Kusini Mashariki mwa Asia. Katika Amerika ya Latini na Karabia, mpango wa eneo wa kushughulikia uchafuzi wa hewa unatekelezwa.

Ustawishaji wa makubaliano ya maeneo ili kushughulikia tatizo linalokithiri mipaka la uchafuzi wa hewa

Katika miaka ya 1960, wanasayansi waligundua kwamba uchafuzi wa hewa, ambao mara nyingi unaanzia umbali wa maelfu ya kilomita, ulikuwa unasababisha ‘mvua ya asidi’ ambayo ilikuwa inaathiri misitu, ikisababisha visiwa vyenye asidi na kupea kwa samaki, na kuhatarisha mifumo mizima ya uhai katika sehemu za Kizio cha Kaskazini hasa katika Scandinavia, Kanada na Scotland.

Makongamano mawili makubwa sana katika miaka ya 70, Kongamano la Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira ya Kibinadamu pamoja na Kongamano la Helsinki kuhusu Usalama na Ushirikiano huko Ulaya, ulitokeza njia ya kuwa na mazungumzo ya makubaliano ya kiserikali ili kupunguza uchafuzi wa hewa.

Mnamo 1979, mataifa 32 yalitia sahihi mkataba wa Kusanyiko la UNECE kuhusu Uchafuzi wa Hewa Ulioenea Sana na Unaokithiri Mipaka: makubaliano ya kwanza ya kimataifa ili kushughulikia uchafuzi wa hewa katika eneo kubwa. Baada ya kuanzisha utekelezaji mwaka wa 1983, Kusanyiko hilo liliweka kanuni za ujumla za ushirikiano wa kimataifa wa kupunguza uchafuzi wa hewa na kuanzisha mfumo wa kitaasisi ambao umeunganisha sayansi na sera.

Matokeo ya kazi hiyo chini ya Kusanyiko kufikia sasa yamekuwa makubwa, yakiwemo miaka 40 ya uzoefu, Vyama 51 katika Kizio cha Kaskazini na Taratibu 8 zinazofanya kazi leo. Kusanyiko hilo ni la kipekee kwa kuwa linaandaa makubaliano ya kimataifa yanayokubalika kisheria, ambayo huweka malengo ya kupunguza viwango lengwa vya vichafuzi kadhaa. Inaandaa nafasi ya mataifa kuzungumzia sera na kubadilishana mazoea bora. Kusanyiko hilo hutegemea makubaliano ya sera dhabiti zinazotegemea sayansi, njia za kuhakikisha nchi zinashirikiana na programu za kutegemeza uwezo wa utendaji.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Mkutano wa Uchafuzi wa Hewa wa Umbali Unaopita Mipaka (UNECE)
  2. Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mazingira ya Kibinadamu (NU)

 

  1. JUKUMU LA KUFUATILIA UBORA WA HEWA NI NINI KATIKA USIMAMIZI WA UBORA WA HEWA?

Kuna changamoto nyingi ambazo nchi hukabili zinaposhughulikia ubora wa hewa. Gharama ya kufuatilia vifaa vilivyoidhinishwa pamoja na kuhakikisha viko sahihi na kuvidumisha, inaweza kuwa mzigo mzito kwa mamlaka nyingi na serikali za kitaifa. Ni muhimu kutambua kwamba gharama ya kufuatilia ubora wa hewa iko chini sana ikilinganishwa na gharama ya kupunguza uchafuzi wa hewa, ya kwanza ikiwa uwekezaji wa umma na ya pili ikiwa uwekezaji wa kibinafsi. Kwa hiyo inayamkinika kwa serikali za kitaifa na miji katika nchi zinazostawi kutanguliza na kuwekeza katika kuanzisha, kuendeleza na kudumisha mitandao ya kufuatilia viwango vya ubora wa hewa yao, ili kupata habari zinazotegemeka za ubora wa hewa.

Nchi nyingi hazina kamwe mitandao ya kufuatilia inayoendeshwa na serikali kwa kutumia vifaa vya kudhibiti kiwango. Katika nchi zenye raslimali chache, mara nyingi vituo vya kufuatilia hupatikana tu katika majiji yao makubwa yenye watu wengi zaidi. Majiji mengi katika nchi zinazostawi yana uwezo wa kuwa tu na kituo kimoja cha kufuatilia au vituo vichache. Hilo ni jambo linalohitaji kushughulikiwa.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Kufuatilia ubora wa hewa (UNEP)
  2. Maendeleo katika ubora wa hewa huko Beijing ni kielelezo kwa miji mingine (CCAC)

 

  1. BIASHARA NA VIWANDA VINAWEZA KUCHUKUA HATUA ZIPI?

Biashara na viwanda vina jukumu zito katika kupunguza uchafuzi wa hewa, kwa sababu nyingi ya shughuli zao ni vyanzo vya aina mbali mbali ya vichafuzi vya hewa. Sekta ya kibinafsi inaweza kuchangia katika uchafuzi wa hewa kupitia utendaji wake mbali mbali na njia za usambazaji kwa sekta tofauti tofauti. Vyanzo vya uchafuzi kutoka kwa sekta za kibinafsi vinahusisha kuchoma fueli, na magari ya kusambaza na usafirishaji. Kwa sababu uchafuzi wa hewa pia unachangia mabadiliko ya tabianchi, kampuni zilizoahidi kupunguza uchafuzi wao wa hewa zinaweza pia kwa wakati huohuo kupunguza kiwango cha kaboni. Ushindi huu maradufu, wa kupunguza uchafuzi wa hewa na kiwango cha kaboni, unaweza na umekuwa kichocheo cha mbinu za kusuluhisha kutoka kwa sekta hiyo. Wakati uliopita, mbinu hizi za kusuluhisha zimekuwa zaidi za kiteknolojia (k.m. kubadili kutoka teknolojia moja hadi nyingine), lakini sehemu nyingine za sekta ya kibinafsi huenda zikahitajika kusonga zaidi ya suluhisho la kiteknolojia. Kuna hatua kadhaa ambazo sekta ya kibinafsi inaweza kuchukua ili kupunguza uchafuzi wa mazingira:

  1. Kutambua na kuweka hesabu ya uchafuzi wa hewa kutoka kwa vituo mbali mbali, hatua za uzalishaji na njia za usambazaji.
  2. Kuanzisha programu zinazopunguza uchafuzi wa hewa, zilizo hususa kwa kila sekta.
  3. uchochea kampeni za kuhamasisha ili kuwasiliana waziwazi kuhusu viwango vya uchafuzi vinavyosababishwa na shughuli zao na kueleza watakachofanya ili kupunguza uchafuzi huo.
  4.  
  5.  
  6.  
  7.  
  8.  
  9.  
  10.  
  11.  
  12.  
  13.  
  14.  
  15.  
  16.  
  17.  
  18.  

Mfano mmoja wa jinsi kiwanda kikubwa kinaweza kutenda ili kupunguza uchafuzi wa hewa umewasilishwa katika ripoti hii ‘Miongozo Inayoweza Kudumishwa ya Uchimbaji wa Boksiti’ ya Taasisi ya Kimataifa ya Alumini (IAI) ambayo inahusisha ubora wa hewa.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Hatua 5 zinazoweza kuchukuliwa na mashirika ya biashara ili kulinda ubora wa hewa yao baada ya janga tandavu la COVID-19 (Jukwaa la Kibiashara la Kidunia)
  2. Kupambana na uchafuzi wa hewa: sehemu ya sekta ya kibinafsi (EDF)

 

  1. NINAWEZA KUFANYA NINI ILI NIBORESHE HEWA KATIKA ENEO LANGU?

Vyanzo vingi vya uchafuzi wa hewa ni vya kimuundo msingi na vinahusiana kabisa na hatua za kiuchumi katika jamii ya kisasa. Kwa hiyo ni vigumu kwa watu binafsi kukomesha uchafuzi wa hewa kivyao. Jitihada ya wengi inahitajika.

Jambo muhimu zaidi ambalo watu wanaweza kufanya ni kupata taarifa kuhusu viwango vya uchafuzi wa hewa mahali wanapoishi na jinsi vinavyowaathiri, na kushinikiza wanasiasa, viongozi na wanaofanya maamuzi ili kupunguza uchafuzi wa hewa katika jiji/ eneo / nchi yao.

Baadhi ya mambo ambayo mtu binafsi anaweza kufanya ili kupunguza mchango wake katika uchafuzi wa hewa ni:

  • kuchagua aina usafiri usichafua mazingira unapopatikana (k.m. usafiri wa umma, kuendesha baiskeli au kutembea badala ya magari ya kibinafsi au pikipiki);
  • ikiwa unafikiria kununua gari, chunguza uchafuzi wake wa nitrojeni dioksidi na chunguza vichafuzi halisi duniani vya gari hilo. Epuka kununua magari ya dizeli. Kununua gari linalotumia mafuta na umeme au gari la umeme pia kutasaidia kupunguza uchafuzi;
  • ikiwa una gari, basi hakikisha linaangaliwa na fundi mara kwa mara ili kupunguza mchango wa gari hilo kwa uchafuzi wa hewa;
  • tumia fueli isiyochafua mazingira na teknolojia kwa ajili ya kupika, mwangaza na kupasha joto;
  • tumia vyanzo vya nishati vinavyoweza kutumiwa tena kila inapowezekana;
  • acha kuchoma uchafu wa nyumbani na wa shambani;
  • acha matumizi ya jiko la kuni;
  • fuatilia mahitaji yako ya nishati na uchafu wa nyumbani na utumie vifaa na balbu zinazotumia kiwango cha chini cha nishati, na mbinu za kupunguza kupoteza joto na madirisha yanayokinza hewa baridi.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Ninaweza kujilindaje kutokana na uchafuzi wa hewa? (Shirika la Mapafu la Uingireza)
  2. Hatua Unazoweza Kuchukua ili Kupunguza Uchafuzi wa Hewa (US EPA)
  3. Njia 10 Unazoweza Kupambana na Uchafuzi wa Hewa (WHO)
  4. Ripoti: Kupumua Hewa Safi Zaidi – Masuluhisho Kumi Yanayoweza Kupimwa kwa Miji Nchini India

 

  1. KUNA UHUSIANO GANI KATI YA UCHAFUZI WA HEWA NA MABADILIKO YA TABIANCHI?

Uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi yana uhusiano wa karibu sana. Vichafuzi vikuu vya hewa vinaathiri hali ya hewa na vingi kati ya hivyo huwa na vyanzo vinavyofanana na gesi ya ukaa (GHGs), hasa zinazohusiana na kuchoma kwa fueli za visukuku. Kadhalika zinaathiriana kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, GHGs, kama vile methani huchangia kufanyizwa kwa kiwango cha chini cha ozoni, na viwango vya chini vya ozoni huongezeka hali joto inapopanda. Kupanda kwa hali joto huongeza mara ambazo mioto ya msituni hutokea, ambayo pia huongeza hata zaidi viwango vya uchafuzi wa hewa.

Kikundi cha vichafuzi kinachoitwa ‘ Vichafuzi vya Muda-Mfupi vya Hali ya Hewa ’ (SLCPs) vinavyotia ndani kaboni nyeusi , ozoni, metheni , na haidroflurokaboni (HFCs) , ni vishinikizi vibaya sana vya anga hewa na – inapohusu ozoni na kaboni nyeusi – ni vichafuzi hatari vya hewa. hatua nyingi za kupunguza SLCP pia hupunguza vichafuzi vingine vya hewa kama vile nitrojeni oksidi. Kwa mfano, hatua za kupunguza kaboni nyeusi huathiri badiliko la hali ya hewa ya eneo na kupunguza kiwango kinachokaribia kufikia kilele cha joto ulimwenguni. Kadhalika, zinapunguza kwa njia kubwa vichafuzi vinavyopelekea PM2.5, hivyo kunufaisha afya ya binadamu. Metheni ni gesi joto hatari sana inayofanyiza ozoni kwenye anga hewa. Hatua za kupunguza metheni, hufaidi jitihada za kuzuia badiliko la hali ya hewa, na kulinda afya ya binadamu na mazao ya mimea. Hatua zinazojumuisha, kama vile zile zinazolenga SLCPs zinaweza kuandaa ushindi mara tatu, kwa kufikia manufaa halisi ya ulimwengu kwa ajili ya afya ya binadamu, kilimo na hali ya hewa.

Uhusiano kati ya uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya hali ya hewa huandaa nafasi ya kuongeza faida za hatua zetu na kuchochea tamaa kubwa hata zaidi za kupunguza. Hivyo mipango na mikakati ya kupunguza joto kwa haraka, lazima ijumuishe hatua za kupunguza vichafuzi vyote na gesi joto zinazochangia matokeo ya hali ya hewa kwa muda mfupi na muda mrefu. Hili litaweka ulimwengu katika hali ambayo inaongeza faida, inapunguza hatari za kutofaulu kwa sera, na kuhakikisha utangulizaji wa maendeleo ya kitaifa.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Vichafuzi vya Muda-Mfupi vya Hali ya Hewa ni Nini? (CCAC)
  2. Maelezo ya jumla ya uchafuzi wa hewa na athari zake (WHO)
  3. Uchafuzi wa Hewa na Afya

 

  1. UCHAFUZI WA HEWA UNAHUSIANA VIPI NA MAENDELEO ENDELEVU?

Uchafuzi wa hewa ni tishio kwa maendeleo endelevu, kwa sababu yanaathiri kwa wakati uleule maswala ya kijamii, kimazingira na kiuchumi yanayohusiana na maendeleo yaliyosawazishwa ya binadamu kama vile afya nzuri, usalama wa chakula, usawa wa kijinsia, udhabiti wa hali ya hewa, na kupunguzwa kwa umaskini.

Maendeleo ya SDGs kadhaa yanahusiana na ubora wa hewa, kama vile SDG lengo 3.9 (afya nzuri na hali njema), SDG lengo 7.1.2 kwa uwezo wa kupata nishati safi ya kupika, SDG lengo 11.6.2 kwa ubora wa hewa katika miji, SDG lengo 11.2 kwa uwezo wa kupata usafiri unaoweza kudumishwa, na SDG 13 (utendaji wa hali ya hewa).

Uchafuzi wa hewa pia huhusiana kimsingi na haki ya jamii na ukosefu wa usawa ulimwenguni. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) , asilimia 97 ya miji katika nchi za mapato ya chini na mapato ya kati, zenye wakaazi zaidi ya 100,000 hazifikii miongozo ya ubora wa hewa. Asilimia hiyo hushuka hadi 49 katika nchi zenye mapato ya juu.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Maelezo ya jumla ya uchafuzi wa hewa na athari zake (WHO)
  2. Uchafuzi wa Hali ya Hewa wa Muda Mfupi na athari zao kwa afya, hali ya hewa, na kilimo (CCAC)
  3. Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa Yanayoweza Kudumishwa (UN)

 

  1. JE, HEWA SAFI NI HAKI YA KIBINADAMU?

Katika angalau nchi 155, mazingira mazuri hutambuliwa kuwa haki kikatiba. Wajibu unaohusiana na hewa safi uko wazi katika vifaa kadhaa vya kimataifa vya haki za kibinadamu, pamoja na Tangazo la Ulimwenguni Kote la Haki za Kibinadamu na Makubaliano ya Kimataifa Kuhusu Haki za Kibiashara, Kijamii na Kitamaduni.

Mwaka wa 2019, katika mkutano wa 40wa Shirika la Haki za Kibinadamu, haki ya kupumua hewa safi iliangaziwa katika ripoti ya Mwanahabari wa Pekee wa Haki za Kibinadamu na Mazingira. Ripoti inaangazia hatua saba ambazo Majimbo lazima yatekeleze , ili kutimiza haki ya kupumua hewa safi.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Shirika la Haki za Kibinadamu hufanya mazungumzo ya majadiliano katika vikundi kuhusu mazingira na makaazi ya kutosha (Shirika la Haki za Kibinadamu la UN)
  2. Hewa safi ikiwa haki ya kibinadamu (UNEP)
  3. Hewa Safi ni Haki ya Kibinadamu – Mwanahabari wa Pekee wa UN
  4. Ripoti ya Kikao cha 40 cha Shirika la Haki za Kibinadamu: Swala la wajibu wa haki za kibinadamu linalohusiana na kufurahia mazingira yaliyo salama, safi, mazuri na yanayoweza kudumishwa (A/HRC/40/55)

 

  1. JE, KUNA UHUSIANO KATI YA HEWA DUNI NA MATOKEO MABAYA SANA YA KIAFYA YA JANGA TANDAVU LA COVID-19?

Uwezekano wa uhusiano kati ya kuwa katika hewa duni na kupatwa na madhara mabaya ya janga tandavu la COVID-19 yanachunguzwa na jamii ya kiafya na kisayansi. Uchafuzi wa hewa unajulikana kuwa na madhara mabaya kwa mfumo wa kupumua na wa moyo na mzunguko wa damu, pamoja na madhara kwa magonjwa mengine ambayo yameonyeshwa kuongeza hali mbaya ya janga tandavu la COVID-19. Ni muhimu kuzingatia ubora wa hewa kama hatua ya ziada ya kusaidia kupunguza mzigo unaowekwa katika afya ya watu na mifumo ya utunzaji afya.

Kadiri uelewaji wetu wa uhusiano huu unavyoboreka, ni muhimu hata zaidi kuazimia kutumia nishati inayoweza kudumishwa kwa muda mrefu, sera za mazingira na viwango vya utekelezaji. Licha ya changamoto kubwa ya ugonjwa huu wa ulimwenguni kote, hatuwezi kuruhusu ipunguze jitihada zetu za kukabiliana na changamoto zisizoepukika, zinazohusiana, na zinazoendelea za mabadiliko ya hali ya hewa, hali duni ya hewa, maendeleo yasiyoweza kudumishwa na kupotezwa kwa uhai mbalimbali.

Kwa taarifa zaidi tazama hapa:

  1. Wanasayansi wanachunguza uhusiano kati ya janga tandavu la Covid-19 na uchafuzi wa hewa unaoangamiza (CCAC)
  2. Uandishi wa Kipekee wa Utafiti wa CCAC kuhusu janga tandavu la COVID-19
  3. Makala: Uchafuzi wa Hewa na janga tandavu la COVID-19: Sehemu ya Vichafuzi katika Kuenea na Kuongezeka kwa Uwezekano wa Kuugua Sana na Kufa Kutokana na janga tandavu la COVID-19 (Comunian S., et al. 2020)
  4. Makala: Athari ya usambazaji hewani wa SARS-CoV-2 kwa janga tandavu la COVID-19. Pitio (Domingo J.L., et al. 2020)