Uchafuzi wa hewa hautambui mipaka ya kitaifa na umeenea kote. Unatuathiri sisi sote na hakuna mtu anayeachwa nyuma kutokana na athari zake. Kaulimbiu ya mwaka huu inaangazia hali ya kuvuka mipaka ya uchafuzi wa hewa na kuangazia umuhimu wa kushirikiana kuwajibika na kuchukua hatua. Pitia orodha ya video za 'Pamoja Kuwa na Hewa Safi’ hapo chini kufahamu ujumbe muhimu kutoka kote ulimwenguni kote.
Kuanzia kwa athari za uchafuzi wa hewa kwa afya yetu, hali ya hewa, bayoanuai, mifumo ya ekolojia hadi kwa suluhisho halisi na la gharama ya chini ya uchafuzi wa hewa kama vile kuboreshwa kwa usalama wa nishati, ubora wa hewa mijini, afya ya binadamu, mifumo nzuri ya ekolojia, kuongezeka kwa mavuno ya kilimo, pitia orodha ya video za #HewaBoraSayariBora hapo chini.
Jumbe kutoka kwa serikali za mtaa, za kikanda na za kitaifa wakati wa maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na angaa za bluu (Septemba 7, 2020).