Wekeza kwa #HewaSafiSasa
Maadhimisho ya tano ya Siku ya Kimaifa ya Hewa Safi ili kuwa na angaa za buluu yatafanyika tarehe 7 Septemba mwaka wa 2024. Siku hii inaangazia umuhimu wa kushughulikia kwa dharura tishio linalobadilika la uchafuzi wa hewa na athari zake mbaya kwa afya, uchumi, na kwa ustahimilifu wa jamii.
Uchafuzi wa hewa umechangia kwa vifo na magonjwa kwa kipindi kirefu na kudhoofisha matarajio ya kiuchumi na ustawi wa jamii. Vyanzo vingi vya uchafuzi wa hewa, kama vile kuchomwa kwa nishati ya visukuku na bayomasi, pia huchangia uzalishaji wa gesi ya ukaa, na kusababisha sayari yetu kupata joto.
Kama mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa hewa huathiri kila mtu lakini huathiri zaidi wajawazito, watoto wachanga na watoto, wazee, wale wanaoishi katika umaskini, na jamii zilizotengwa kihistoria. Ukubwa na upesi wa changamoto hizi hauwezi kupuuzwa.
Siku inayoadhimishwa chini ya kaulimbiu ya "wekeza kwa #HewaSafiSasa", maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia umuhimu wa kuimarisha uwekezaji, sera thabiti, na uwajibikaji wa pamoja ili kukomesha uchafuzi wa hewa kwa dharura. Ni tishio la pili kwa ukubwa linalosababisha vifo, na kusababisha vifo vya mapema vya takriban watu milioni 8.1 vinavyotokana na magonjwa kama vile kiharusi, ugonjwa wa moyo, saratani ya mapafu na maambukizi makali ya mfumo wa kupumulia.
Takwimu hutusaidia kufahamu ukubwa wa suala hili: asilimia 99 ya watu duniani kote huvuta hewa chafu; uchafuzi wa hewa ulisababisha vifo milioni 8.1 katika mwaka wa 2021, huku zaidi ya asilimia 90 ikihusishwa na magonjwa yasiyoambukizaza; na zaidi ya watoto 700,000 chini ya miaka mitano wakifariki kutokana na sababu zinazohusiana na uchafuzi wa hewa wa majumbani na nje.
Tukichukua hatua sasa, tunaweza kupunguza kwa nusu hasara ya mazao duniani kutokana na vichafuzi vya hewa kufikia mwaka wa 2050. Kupunguza uzalizaji wa methani, gesi kuu ya kaa na inayochafua hewa, kunaweza kuokoa kati ya dola bilioni 4 hadi bilioni 33. Gharama ya kutochukua hatua ni ya kushangaza, huku uchafuzi wa hewa ukikadiriwa kugharimu uchumi wa dunia $8.1 trilioni kwa mwaka, sawa na 6.1% ya Pato la Taifa la kimataifa kutokana na kuongezeka kwa gharama za huduma za afya.
Jiunge na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za bluu kwa kwa kushiriki juhudi zako kwa mitandao ya kijamii kwa kutumia hashitagi #HewaSafiSasa na #SikuyaHewaSafiDuniani.
Watu wanaweza kushiriki maoni yao kuhusu Hewa Safi ili kuwa na anga za bluu kwa kushiriki juhudi zao kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia hashitagi #HewaSafiSasa na #SikuyaHewaSafiDuniani.