Maelezo ya Jumla

Jukwaa la uchukuaji wa hatua 

Maadhimisho ya tano ya Siku ya Kimaifa ya Hewa Safi ili kuwa na angaa za buluu yatafanyika tarehe 7 Septemba mwaka wa 2024.

Inaadhimishwa chini ya kaulimbiu ya "wekeza kwa #HewaSafiSasa" na inaangazia umuhimu wa kuimarisha uwekezaji, sera thabiti,  na uwajibikaji wa pamoja ili kukomesha uchafuzi wa hewa na athari zake kwa afya, uchumi, na kwa hali ya hewa. 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitenga tarehe 7 Septemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu katika mwaka  wa 2019, na maadhimisho ya kwanza yalifanyika mwaka wa 2020. Hii inafuatia ongezeko la uelewa wa jamii ya kimataifa kuhusu hatari za uchafuzi wa hewa na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha juhudi za kuboresha hali ya hewa ili kutunza afya ya binadamu na hali ya mazingira.

Uchafuzi wa hewa ni tishio la mazingira sio tu kwa afya ya binadamu, bali pia kwa hali ya sayari. Una madhara mabaya kwa hali ya hewa, bayoanuai na kwa mifumo ya ekolojia. Kuwekeza kwa hewa safi kunaweza okoa mamilioni ya watu, kukabiliana na mabadiliko ya tabiachi, kukuza jamii zilizo na usawa zaidi na kuimarisha uchumi. Mazingira salama, safi, bora na endelevu, ikijumuisha hewa safi, ni nguzo ya kujivunia nyingi ya haki za binadamu.

Uchafuzi wa hewa huathiri kwa kiwango kikubwa watoto na wazee, na huwa na athari mbaya kwa mifumo ya ekolojia. Kuboresha hali ya hewa ni muhimu ili kukabiliana na athari za vichafuzi vingi vinavyochangia moja kwa moja kwa janga la mabadiliko ya tabianchi. Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, pia inatambua kwamba kupunguza uchafuzi wa hewa ni muhimu ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu inakusudia kujenga jamii ya kimataifa ya kuchukua hatua inayohimiza nchi kushirikiana ili kukabiliana na uchafuzi wa hewa ili kuhakikishia kuwa tunatunza mifumo yetu ya ekolojia. Kufanikisha haya, inawapa watu jukwaa linalowezesha ushirikiano katika ngazi ya mtu binafsi, kitaifa, kikanda na kimataifa kufanya kazi pamoja na Kuwekeza  kwa #HewaSafiSasa.