HISTORIA
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitenga tarehe 7 Septemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu katika mwaka wa 2019, na maadhimisho ya kwanza yalifanyika mwaka wa 2020. Hii inafuatia ongezeko la ufahamu wa jamii ya kimataifa kuhusu hatari za uchafuzi wa hewa na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha juhudi za kuboresha hali ya hewa ili kutunza afya ya binadamu na hali ya mazingira.
2023:
Kaulimbiu ya maadhimisho ya nne ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu ni “Pamoja Kuwa na Hewa Safi. Kaulimbiu hii inaangazia umuhimu wa kuwa na ushirikiano thabiti, kuimarisha uwekezaji na uwajibikaji wa pamoja ili kukomesha uchafuzi wa hewa. Pia inaangazia umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika ya maendeleo, sekta ya kibinafsi, na mashirika ya uraia katika kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuboresha hali ya hewa.
2022:
Kaulimbiu ya maadhimisho ya tatu ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu ilikuwa “Hewa Yetu Sote”. Kaulimbiu hii iliangazia hali ya kuvuka mipaka ya uchafuzi wa hewa, na kusisitiza umuhimu wa uwajibikaji wa pamoja na kuchukua hatua. Pia inaangazia umuhimu wa ushirikiano wa dharura uliowekewa mikakati wa kimataifa na kikanda ili kuwa na utekelezaji bora zaidi wa sera na hatua za kukabiliana na uchafuzi wa hewa.
Siku hiyo ilishuhudia mashirika na watu wa tabaka mbalimbali wakiomba kufanya kazi pamoja nyumbani na katika sehemu zetu za kazi, jumuiya, serikali na mipakani ili kuboresha hali ya hewa yetu. Uchafuzi wa mazingira ni tatizo la kimataifa ambalo ni lazima tuchukue hatua pamoja ili kulikabili. Inafuata kutoka kwa mada ya 2021 ya "Hewa Bora, Sayari Bora". Ripoti kuhusu maadhimisho ya Siku hiyo inapatikana kupitia link.
2021:
Kaulimbiu ya maadhimisho ya pili ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu ilikuwa “Hewa Bora, Sayari Bora”. Siku hiyo ililenga kumfanya kila mtu kutafakari kuhusu hali halisi ya kimataifa ya uchafuzi wa mazingira, ikihusishwa sio tu na afya ya binadamu, bali pia na ya sayari yetu. Uchafuzi wa mazingira hushuhudiwa kote ulimwenguni, kwa hivyo kufikiria tu kuhusu eneo lako hakuwezi kutatua tatizo.
Serikali, mashirika na watu kutoka kote ulimwenguni waliungana kushiriki katika maadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu. Muhtasari wa kina wa shughuli zote unaweza kupatikana hapa.
2020:
Umoja wa Mataifa ulizindua Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu tarehe 7 Septemba mwaka wa 2020 chini ya kaulimbiu ya "Hewa Safi Kwa Wote". Ililenga kujenga jamii ya kimataifa ya kuchukua hatua ili kuhimiza ushirikiano katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa, na kutoa wito kwa nchi kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na uchafuzi wa hewa na kutoa hewa safi kwa kila mtu.
Kuzindua Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili ukwa anga za buluu, UNEP, kwa msaada kutoka kwa wabia, ilichukua jukumu la kuweka msingi muhimu, uratibu na ushirikiano mpana ili kuwezesha maadhimisho yenye mafanikio na ya kusisimua, ikiwa ni pamoja na kukuza nyenzo muhimu za mawasiliano na utambulisho thabiti unaoonekana, nembo na chapa zitakazoenziwa kwa miongo kadhaa ijayo. Baadhi ya mambo muhimu yanaweza kutazamwa hapa.