Hewa Safi na SDGs

 

Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanalenga kumaliza umaskini uliokithiri na kuunda ulimwengu safi na endelevu kufikia mwaka mwa 2030. Katika msingi wake kuna afya na ustawi wa watu na sayari yetu, na kufanya uchafuzi wa hewa tishio kuu la kutimiza maono ya ulimwengu bora. Kukabiliana na uchafuzi wa hewa kunaweza kunaweza kushughulikia malengo mengine mahususi. Kwa njia hii:

Lengo la 1 linalenga kutokomeza umaskini. Watu wanaoishi katika umaskini mara nyingi hutegemea fueli inayopatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu inayochafua mazingira kupikia na kupasha joto, na kusababisha kuongezeka kwa uchafuzi wa hewa na uwezekano wa kuathirika na madhara yake. Juhudi za kutokomeza umaskini kwa hiyo zinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa ubora wa hewa na kama sivyo, kinyume chake kitatokea.

Lengo la 2 linalenga kutokomeza njaa. Uchafuzi wa hewa huharibu mimea na kupunguza uzalishaji wa kilimo, na hivyo kuwa tishio kubwa kwa utoshelezaji wa chakula duniani.  Tunaweza kupunguza uharibifu wa mimea duniani kwa nusu tukipunguza uzalishaji wa methani. Uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi huathiri mfumo wa chakula duniani kwa njia ambayo wale wanaokabiliwa na njaa na utapiamlo pia wako hatari zaidi kwa matishio haya ya ziada. Ili kumaliza njaa lazima tukabiliane na majanga haya yanayoingiliana.

Lengo la 3 linalenga afya njema na ustawi kwa wote — nguzo ya kuwezesha watu kufikia malengo yao shuleni, kazini na nyumbani. Kila hatua tunayochukua kukabiliana na uchafuzi wa hewa ni hatua kuelekea kufikia lengo hili.

Lengo la 5 linalenga usawa wa kijinsia. Wanawake na wasichana, hasa katika nchi za kipato cha chini na cha kati na maeneo ya vijijini, wana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na uchafuzi wa mazingira kutokana na nishati ya kupikia inayochafua mazingira. Kujengea wanawake uwezo wa haki za kifedha na teknolojia, kama ilivyoainishwa katika shabaha 5.A na 5.B, kunaweza kutekeleza wajibu muhimu wa kupunguza uchafuzi wa hewa na kuboresha matokeo ya afya kwa wanawake.

Lengo la 7 linalenga upatikanaji wa nishati isiyochafua mazingira kwa bei nafuu- ambayo ni muhimu ili kuondoa watu kutoka kwa umaskini na kuwezesha maendeleo endelevu ya uchumi. Watu bilioni tatu wanapika na kupasha joto nyumba zao na fueli inayochafua mazingira. Matokeo yake ni vifo vya watu takribani milioni 4 kila mwaka, haswa wanawake na watoto. Nishati isiyochafua mazingira na inayoweza kutumika tena itaokoa maisha na kukuza maendeleo ya uchumi.

Lengo la 9 linaangazia viwanda, uvumbuzi na miundomsingi. Lengo la 9.4 linalenga kufanya viwanda kuwa endelevu zaidi kwa kutumia teknolojia isiyochafua mazingira na inayojali mazingira na kuboresha matumizi ya rasilimali kikamilifu. Viwanda kuacha kutumia nishati ya visukuku na kuanza kutumia teknolojia isiochafua mazingira kunaweza kuboresha hali yaa hewa kwa kiwango kikubwa.

Lengo la 11 la miji na jamii endelevu ni muhimu katika ulimwengu wetu unaoendelea kukuza miji. Miji huchangia asilimia 75 ya uzalishaji wa hewa ya ukaa na asilimia 70 ya jumla ya idadi ya watu duniani wataishi mijini kufikia mwaka wa 2050. Sera zinazofanya miji kuwa ya kisasa, thabiti na ya kijani kibichi — kupitia kupanga miji, teknolojia na ushirikishaji wa raia — zinaweza kutoa hali bora ya hewa na kubadilisha mazingira ya mijini.

Lengo la 12 linakuza uzalishaji na matumizi ya bidhaa kwa njia ya kuwajibika. Lengo la 12.4 linasisitiza uboreshaji wa ushughulikiaji wa kemikali na taka, hali inayoweza kupunguza uzalishaji wa hewa chafu angani. Mbinu bora za usimamizi wa taka zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli kama vile uchomaji taka.

Lengo la13 linashughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi. Vichafuzi vingi vya hewa vinavyoathiri afya zetu pia huongeza joto angani. Vitendo vya kuboresha hali ya hewa-kama vile kuanza kutumia nishati isiyochafua mazingira, suluhisho la upishi na uchukuzi-pia vitashughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi.

Lengo la 17

linasisitiza umuhimu wa ushirikiano ili kufikia malengo haya. Juhudi za ushirikiano kati ya serikali, viwanda na jamii ni muhimu ili kupunguza uchafuzi wa hewa na kutimiza Ajenda pana ya 2030.