Hewa safi ni haki ya binadamu
Katika angalau mataifa 155, mazingira mazuri hutambuliwa kama haki ya kikatiba. Majukumu yanayohusiana na hewa safi yamewekwa katika vyombo kadhaa vya haki za kibinadamu vya kimataifa, ikijumuisha Tamko la Haki za Binadamu na Makubaliano ya Kimataifa Kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni.
Haki ya kupumua hewa safi ina uhusiano wa moja kwa moja na kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ikiwa ni pamoja na maisha yenye afya, miji endelevu, uwezo wa kupata nishati isiyochafua mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Safisha Hewa
Idadi ya watu inapoelekea kuwa bilioni 10 wengi wao wakiwa mijini, uchafuzi wa hewa unaweza kuwa mbaya zaidi. Serikali zimejitolea kusafisha hewa na ni suala lililopewa kipaumbele na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.
Mnamo tarehe moja Septemba UNEP ilizindua ‘Safisha Hewa’ kama sehemu ya kampeni ya #KomeshaUchafuzi. ‘Safisha Hewa’ inalenga kuhamasisha kuhusu athari ya uchafuzi wa hewa kwa afya ya binadamu na kwa mazingira na uchumi wao. Pia inalenga kutoa suluhu kutoka kwa watu binafsi ili kuboresha ubora wa hewa katika maeneo wanayoishi.
Jifahamishe zaidi kuhusu kampeni ya Safisha Hewa hapa.