Wakati wa maadhimisho ya tano ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za buluu, ni wakati wa kukuza ushirikiano wa wadau mbalimbali, kuimarisha uwekezaji na kukumbatia wajibu wetu wa pamoja wa kushughulikia uchafuzi wa hewa. Ni wakati wa kuwekeza kwa #HewaSafiSasa.
Tunapoelekea #SikuYaHewaSafiDuniani, tunaangazia yaliojiri kutoka kwa Mfumo wa Umoja wa Mataifa, washirika wake na wengine wanaosaidia kuangazia athari mbaya za uchafuzi wa hewa kwa afya ya binadamu, kwa hali ya hewa, kwa bayoanuai na kwa mifumo ya ekolojia, na kwa hali ya maisha kwa ujumla.