7 September 2020 Maadhimsho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi inatoa wito wa kufanya uamuzi wa kimataifa wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa

Matukio ya hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa yanapoendelea kuongezeka, juhudi za kimataifa za kupunguza uchafuzi wa hewa na athari zake zitaimarishwa kupitia uhamasishaji, kwa mara ya kwanza kabisa, dunia inapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu tarehe 7 Septemba.

Toleo la habari

Nairobi, Septemba 7, 2020 - Matukio ya hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa yanapoendelea kuongezeka, juhudi za kimataifa za kupunguza uchafuzi wa hewa na athari zake zitaimarishwa kupitia uhamasishaji, kwa mara ya kwanza kabisa, dunia inapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu tarehe 7 Septemba.

Siku iliyoidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 2019, Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu - ambayo kuadhimishwa kwake kutaendeshwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)- inaonyesha umuhimu wa kufanya uhamasishaji kwa dharura katika ngazi zote na kukuza na kuendeleza hatua za kuimarisha ubora wa hewa. Serikali ya Korea ilikuwa mustari mbele katika juhudi zi kimataifa za kubuni siku hii mpya, Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu na itandaa hafla ya kuanzia maadhimisho.

Katika maeneo mengi ulimwenguni, matukio ya hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa hotekea katika misimu, yamekuwa yanatokea kama vile misimu ya monsuni au vuli. Mwanzoni mwa mwezi wa Novemba, New Delhi na miji mingine kaskazini mwa India ilishuhudia kiwango cha uchafuzi wa hewa kilichopelekea safari za ndege kusitishwa kwa mda na kuwalazimisha watu kusalia majumbao mwao huku wakivalia barakoa. Mjini Ulaanbaatar, nchini Mongolia, na katika mji mkuu wa Thai, Bangkok, matukio haya hutokea Januari na Februari. Mjini California na nchini Australia, mioto ya porini inayotekea katika msimu wa majira ya joto, inayochongewa na mabadiliko ya tabianchi, huharibu maeneo ya makazi na kuenea kwa kasi.

Hii ni mifano ya athari mbaya mno za janga linalotuathiri sote – uchafuzi wa hewa huathiri wanadamu, wanyama na sayari, huku ikikadiriwa kuwa watu million 7 hufa mapema kutokana na magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa hewa. Uchafuzi wa hewa, ni hatari inayotokana na mazingira inayoathiri afya ya binadamu na mojawapo ya vyanzo vya magonjwa na vifo vinavyoweza kuzuiliwa kote duniani. Kila mwaka. Mamilioni ya watu wanaoishi na magonjwa haya hukumbwa na kiwango fulani cha ulemavu. 

"Kote ulimwenguni, tisa kati ya kila watu kumi hupumua hewa chafu," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema katika ujumbe aliotoa leo. "Kiwango cha changamoto hii kinahitaji hatua za uamuzi kutoka kwa serikali, mashirika ya biashara na jamii kokomesha kutegemea visukuku kama fueli na kuegemea matumizi ya nishati jadidifu, isiyochafua mazingira, inayopatikana kwa bei nafuu. Wakati wa maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu, tujitolee kutotumia tena makaa ya mawe, ili kukuza chumi zisizochafua mazingira zitakazotuhakikishia afya njema.

Uchafuzi wa hewa siyo tishio tu kwa afya ya binadamu lakini pia inadhuru mimea na mifumo ya ekoloja. Uchafuzi wa hewa unasababishwa na ozoni hupelekea hasara ya mimea ya tani milioni 52 kote ulimwenguni kila mwaka. Uchafuzi wa hewa pia huchombea changamoto ya hali ya hewa huku uzalishaji wa gesi ya ukaa na vichafuzi vya hewa vikisababishwa na vyanzo vile vile. Hii inamanisha kuwa uchafuzi wa hewa siyo hatari tu kwa afya ya binadamu na kwa kiwango cha maisha kwa sasa, lakini pia huhatarisha maisha ya vizazi vijavyo.

Mheshimiwa Moon Jae-in, Rais wa Jamhuri ya Korea, alisema: "Nina furaha isiyokuwa na kifani kusherehekea maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu, siku iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana. Nina matumaini kuwa tukio hili litaimarisha uhamasishaji wa kimataifa kuhusu uchafuzi wa hewa unaovuka mipakaa na kuwa nguzo muhimu katika juhudi za kimataifa ili kupata masuluhisho ya kuwezesha kuwepo kwa hewa safi."

Habari njema ni kuwa ni masuluhisho yanayowezekana na yanayopatikana kwa bei nafuu yanayowezesha kupunguza uchafuzi wa hewa. Uchafuzi wa hewa hauheshimu mipaka ya kimataifa na kwa hivyo, nchi ni sharti zishirikiane kutoa kipaumbele hatua za kupunguza uchafuzi wa hewa na kuwekeza katuka suluhu isiyochafua mazingira; utafiti unaonyesha kuwa nishati jadidifu inapatikana kwa bei nafuu kuliko kipindi kingine chochote.

Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu inatoa wito wa kuimarisha ushirikiano duniani katika ngazi ya kimataifa, ya kikanda na ya kimaeneo. Inatoa fursa ya kuimarisha mshikamano wa kimataifa na kumairisha umaarufu wa kuchukua hatua za kisiasa dhidi ya uchafuzi wa hewa na mabadilko ya tabianchi, ikijumuisha hatua kama vile kuimarisha ukusanyaji wa data kuhusu ubora wa hewa, kushirikiana kufanya utafiti, kubuni teknolojia mpya na kushiriki matendo bora zaidi.

"Uchafuzi wa hewa ni changamoto inayotokana na mazingira iliyo na madhara makubwa kwa afya ya binadamu. Huathiri maskini kwa viwango vinavyotofautiana. Gharama kwa uchumi zinaongezeka - iwe kupitia kwa gharama za matibabu, kupungua kwa uwezo wa kuzalisha, kupungua kwa mazao ya mimea au kupungua kwa ushindani kati ya miji," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Masharti ya kudhibiti shughuli wakati wa COVID-19 yameonyesha kuwa kuna uwezekano wa kutokuwa na ukungu angani. Eti watu wako tayari kusikiliza wanasayansi. Eti tuna uwezo wa kuchukua hatua kwa haraka ili kutunza afya ya binadamu. Ni sharti tuchukue hatua za aina hiyo kwa dharura ili kuepuka ukungu unatokana na uchafuzi wa hewa. Tukifanya hivyo, tunaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu na kuokoa mabilioni ya dola kila mwaka."

"Kutokana na changamoto za kimataifa zinazotokana na uchafuzi wa hewa, mabadiliko ya tabianchi, ubaguzi wa kijamii na kiuchumi, na ugonjwa mtandavu unaondelea kushuhudiwa wa COVID-19, tuna uwezo wa kujiimarisha baada ya janga hili," amesema Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO. "Serikali nyingi tayari zimechukua hatua za kujumuisha afya, uchafuzi wa hewa na hali ya hewa katika sera zake. Sasa ni wakati wa kutafakari tena kuhusu jinsi tunavyoweza kutoa mpangilio kwa jamii zetu, miji zetu, usafiri wetu, na jinsi ya kupika na kupasha joto majumbani mwetu -kwa manufaa ya afya.

Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu itasherehekewa kupitia shughuli mbalimbali kote ulimwenguni, ikijumuisha sherehe rasmi ya ufunguzi, mgeni rasmi akiwa Rais Moon Jae-in waJamhuri ya Korea; Jukwaa la Kimataifa la Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu litakaloendeshwa na Ban Ki-moon, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, sasa yeye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kimataifa ya Korea kuhusu Hali ya Hewa na Ubora wa Hewa na hafla ya UNEP ikiongozwa na Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP atakayesaidiwa na Waziri wa Mazingira wa Korea, Cho Myung-Rae  na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus. Taarifa zaidi kuhusu shughuli hizi kote ulimwenguni hapa.

MAKALA KWA WAHARIRI

Ufadhili wa kufanikisha Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu ulitoka kwa GIZ. Uratibu na mpangilio ilifanywa na UNEP na Muungano wa Hali ya Hewa na Hewa Safi.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

(UNEP) ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo wa Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

Tiy Chung, Afisa wa Mawasiliano, Climate and Clean Air Coalition, [email protected]

Последние истории
Пресс-релиз

Согласно новым данным Программы ООН по окружающей среде (ЮНЕП), высокотехнологичная система, которая выявляет крупные утечки метана, за последние…

Пресс-релиз

Найроби, 7 сентября 2024 г. Сегодня мир отмечает пятый ежегодный Международный день чистого воздуха для голубого неба, призывая к начать…